SOMA HAPA KAMA UNAJIANDA NA USAILI NEC

 


Uboreshaji wa Daftari

Kwa mujibu wa Kifungu cha 16 (5) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024, Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utakuwa mara mbili kati ya kipindi kinachoanza mara baada ya uchaguzi mkuu na kabla ya siku ya uteuzi. Wanaohusika katika zoezi hili ni wananchi ambao: -

  1. Wametimiza umri wa miaka 18 na kuendelea ambao hawakuandikishwa hapo awali;
  2. Watakaotimiza miaka 18 kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025;
  3. Waliojiandikisha awali na wamehama Kata au Jimbo moja kwenda jingine;
  4. Waliopoteza sifa mfano wale waliofariki kuondolewa katika Daftari;
  5. Wenye taarifa zilizokosewa wakati wa uandikishaji; na
  6. Waliopoteza au kadi zao kuharibika.

Watendaji wa Uandikishaji/ Uboreshaji

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi hutumia watendaji mbalimbali wakati wa Uandikishaji na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Watendaji hawa ni pamoja na:-

  1. Waratibu wa Uchaguzi wa Mkoa;
  2. Maafisa Waandikishaji;
  3. Maafisa Waandikishaji Wasaidizi;
  4. Waandishi Wasaidizi; na
  5. Mwenyesha Kifaa cha Bayometriki

Mawakala wa Uandikishaji wa Wapiga Kura

Kwa mujibu wa Kifungu cha 17 (1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024, Chama cha Siasa chenye usajili wa kudumu kinaweza kumteua mtu mmoja katika kila kituo cha uandikishaji kuwa Wakala wa Uandikishaji wa Wapiga Kura.

Wajibu/Majukumu ya Mawakala wa Uandikishaji

  1. Kufuatilia zoezi la uboreshaji na kutazama kama linazingatia Sheria, Kanuni na Maelekezo ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
  2. Kushirikiana na Waandishi Wasaidizi kutambua wakazi wa eneo hilo na kutoa taarifa juu ya watu wasio na sifa.

Pamoja na majukumu tajwa, Mawakala wa Uboreshaji hawaruhusiwi kufanya yafuatayo:-

  1. Kuingilia shughuli za uendeshaji wa zoezi la Uboreshaji. Msimamizi wa kituo ndiye mwenye mamlaka ya mwisho juu ya nani anastahili kuandikishwa au kuboresha taarifa zake kwa mujibu wa Sheria.
  2. Kufanya kampeni za kisiasa katika kituo cha uandikishaji
  3. Kuorodhesha majina ya watu wanaojiandikisha.

Kiapo cha Kutunza Siri cha Mawakala wa Uandikishaji

Kila Wakala wa Uandikishaji kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria, ni lazima kula kiapo cha kutunza siri za taarifa za mwombaji au Mpiga Kura aliyeandikishwa. Wakala atakula kiapo mbele ya Afisa Mwandikishaji au Afisa Mwandikishaji Msaidizi. Hata hivyo, kutokuwepo kwa Wakala wa uandikishaji katika kituo cha kuandikisha Wapiga Kura hakuzuii utekelezaji wa majukumu ya Uandikishaji Wapiga Kura.

Watazamaji wa Uandikishaji

Kwa mujibu wa Kanuni za 46, 47, 48, 49, 50 na 51 (1) za Kanuni za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura za Mwaka 2024 zilizoandaliwa chini ya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024  Watazamaji wa ndani na kimataifa, wanaruhusiwa kutazama mchakato wa Uboreshaji utakavyofanyika katika vituo vya Uandikishaji.

Watazamaji wa Uandikishaji kabla ya kuanza kutembelea vituo vya Uandikishaji, ni lazima waombe na kupatiwa idhini ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kuwa Watazamaji. Aidha, Watazamaji 24 watakaoruhusiwa na Tume watapewa barua za kuwatambulisha kwa Maafisa Waandikishaji na Mwongozo wa watazamaji wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ulioandaliwa na Tume. Maafisa Waandikishaji watatakiwa kuwapa barua za kuwatambulisha kwa Watendaji wa vituo ambavyo watavitembelea. Aidha, Watazamaji wa Uandikishaji wa Wapiga Kura hawapaswi kutoa maelekezo kwa Mwandishi Msaidizi katika kituo husika.

Kuweka Wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura

Kwa mujibu wa Kifungu vya 11 (2) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024, Tume inatakiwa kuweka wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura ili kutoa fursa kwa wananchi:

  1. Kulikagua Daftari;
  2. Kufanya marekebisho ya majina au mahali wanapoishi;
  3. Kuingiza au kufuta majina ya Wapiga Kura;
  4. Kuweka pingamizi kwa Mpiga Kura aliyeandikishwa na hana sifa za kuwemo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Kumuwekea Pingamizi aliyeandikishwa kwenye Daftari la Awali

Kifungu cha 27 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024,kinaruhusu Mkurugenzi wa Uchaguzi au Afisa Mwandikishaji au mtu yeyote aliyeandikishwa kuwa Mpiga Kura, kuweka pingamizi dhidi ya jina lililopo katika Daftari la Awali la Wapiga Kura. Kifungu cha 28 Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024,  kinaweka utaratibu wa kuweka pingamizi. Mtu aliyewekewa pingamizi hutakiwa kupelekewa taarifa ili aweze kutoa ufafanuzi ndani ya siku saba (7).

Kifungu cha 29 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024 Mahakama itapaswa kutoa uamuzi wa rufaa hiyo ndani ya siku 14 tangu tarehe ya kupokea rufaa hiyo, uamuzi wa Mahakama ya Wilaya na iwapo aliyewekewa pingamizi hakubaliani na 25 maamuzi ya Afisa Mwandikishaji ya kuendelea kukataliwa kuwemo katika Daftari, ana haki ya kukata rufaa dhidi ya maamuzi Wilaya ndiyo utakuwa uamuzi wa mwisho na mtu hatoweza kukata rufaa katika Mahakama nyingine yoyote.

 

Uwekaji Wazi Daftari la Awali 

Kwa mujibu wa Kifungu cha 24 (2) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024, Afisa mwandikishaji ataweka wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura katika kila kata na, ikilazimu, anaweza kufanya marekebisho kwa namna itakavyoelekezwa na Tume. Aidha Kifungu cha 34 cha Kanuni za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura za Mwaka 2024,  Tume au Mkurugenzi wa Uchaguzi, afisa mwandikishaji ataweka au kuwezesha kuwekwa wazi kwa Daftari la Awali la Wapiga Kura kwa kila kata kwa ajili ya kukaguliwa na umma katika muda utakaoamuliwa na Tume. Tume huweka wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura ili kutoa fursa kwa wananchi:

  1. Kulikagua Daftari;
  2. Kufanya marekebisho ya majina au mahali wanapoishi;
  3. Kuingiza au kufuta majina ya Wapiga Kura;
  4. Kuweka pingamizi kwa Mpiga Kura aliyeandikishwa na hana sifa za kuwemo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Kumuwekea Pingamizi aliyeandikishwa kwenye Daftari la Awali

Kwa mujibu wa Kifungu cha 26 (1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024, Mtu ambaye jina lake lipo katika Daftari la Awali la Wapiga Kura la eneo lolote la uchaguzi anaweza kupinga kuendelea kuwemo kwa jina lake mwenyewe au jina la mtu mwingine yeyote katika Daftari la Awali la Wapiga Kura kwa sababu yeye au mtu huyo mwingine hana sifa au amepoteza sifa za kuandikishwa au mtu huyo mwingine amefariki. (2) Mtu anayeweka pingamizi chini ya kifungu hiki atajulikana kama “mweka pingamizi”

Kifungu cha 27(1), (2) na (3) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024, kila pingamizi litawekwa kwa kujaza nakala mbili za fomu iliyoainishwa na litawasilishwa kwa afisa mwandikishaji ndani ya muda ulioainishwa. Kila pingamizi, litawasilishwa likiambatishwa na malipo ya dhamana ya kiasi cha fedha kitakachoainishwa na Tume kwa notisi itakayochapishwa katika Gazeti la Serikali. Afisa mwandikishaji, mapema iwezekanavyo baada ya kupokea pingamizi lililowekwa kwa mujibu wa Sehemu hii, atapeleka taarifa ya pingamizi hilo kwa mtu aliyewekewa pingamizi: Isipokuwa kwamba, afisa mwandikishaji atapaswa kubandika taarifa ya pingamizi katika mbao za matangazo katika kituo cha uandikishaji endapo pingamizi limewekwa kwa sababu mtu ambaye jina lake limo katika Daftari la Awali la Wapiga Kura amefariki.

Kifungu cha 29  (1) na (2) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024, endapo mweka pingamizi au mtu aliyewekewa pingamizi hataridhika na uamuzi wa afisa mwandikishaji chini ya kifungu cha 28, mweka pingamizi au mtu huyo anaweza, ndani ya siku saba tangu tarehe ya uamuzi huo kutolewa, kukata rufaa katika Mahakama ya Mwanzo. Mahakama ya Mwanzo itatoa uamuzi wa rufaa ndani ya siku kumi na nne tangu siku rufaa ilipowasilishwa.


BAADHI YA MASWALI YALIYO ULIZWA KWA WALIO FANYA USAILI TAYARI



 

Post a Comment

0 Comments